Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, ameonekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, na kuweka wazi uwezekano wa kuwania tena Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2024.
Akizungumza katika mkutano wa kisiasa wa Muungano wa Kihafidhina (CPAC) uliofanyika mjini Orlando katika jimbo la Florida, mwanachama huyo wa Republican amesema huenda akajitosa tena katika kinya’nganyiro cha Urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Akiashiria uwezekano huo, Trump aliyeiongoza Marekani kwa muhula mmoja kuanzia mwaka 2017 hadi 2021 amesema:
“Nani anayejua. Ninaweza kuamua kuwashinda kwa mara ya tatu. Hio ni sawa?,” Trump
Trump pia amesisitiza madai yake yasiokuwa na ushahidi kuwa alimshinda Rais wa sasa Joe Biden katika uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka jana.