Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema maeneo ya vijijini yanakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji hivyo zinahitajika juhudi kubwa kuhakikisha huduma inafikishwa kwa wakati katika maeneo hayo jambo ambalo linategemea upatikanaji wa vifaa vyenye kutosheleza na viwango vya ubora ikiwemo mabomba.
Waziri Aweso ametoa kauli hiyo Jijini DSM akiwa kwenye ziara ya kutembelea viwanda vinavyozalisha mabomba ya maji ili kujiridhisha uwezo wa uzalishaji endapo unatosheleza mahitaji ya ndani jambo ambalo litaondoa visingizio vya ucheleweshwaji wa miradi kwa wakandarasi waliopewa zabuni ya kutekeleza miradi mbalimbali kwa kuwa mabomba yanayotumika kusambaza maji yanapatikana hapa hapa nchini.
Waziri Awesso ameagiza Bilion 1 zilipwe kwa kiwanda cha Simba Plastick ambacho kimepewa kazi ya usambazaji wa mabomba katika mradi wa Kyaka-Nyakanazi huku Mkurugenzi mkuu wakala wa maji Vijijini Ruwasa Mhandisi Clement Kivegalo akivitaka viwanda hivyo kuongeza uzalishaji ili uweze kwenda na kasi ya utekelezwaji wa miradi katika maeneo ya vijijini nchi nzima.