Watu 20 wamefariki dunia huku wengine zaidi ya 600 wakijeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea nchini Equatorial Guinea jana jumapili.
Mlipuko huo umetokea karibu na kambi za wanajeshi mji mkuu wa Bata ambao ni maarufu kwa mafuta na gesi ukiwa na wakazi milioni 1.4
Rais wa Equitorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema amenukuliwa na mitandao mbali mbali akisema mlipuko huo umesababishwa na uzembe uliohusishwa na huifadhi baruti kali kambini.
Aliongeza kwamba huenda tukio hilo limetokea kufuatia hatua ya wakulima kuchoma mashamba yanayozunguka kambi za jeshi.
Naye Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Colonel Remy Lamah kupitia mtandao wake wa Twitter anaomba wahudumu wa afya kujitolea na kwenda katika hospitali ya eneo la Bata. Pia ametoa wito watu kujitolea kutoa damu kwa sababu ya idadi kubwa ya waliojeruhiwa