Rais wa TFF Wallace Karia amethibitisha kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha kugombea Ujumbe wa Baraza la FIFA kuwakilisha nchi zinazozungumza lugha ya Kiingereza.
“Ni kweli, nafasi za kuingia kutoka Afrika zinagombewa kutokana na uzungumzwaji wa lugha, sisi tulikuwa tunagombea nafasi za kuingia kwa lugha ya Kiingereza [Anglophone].
“Kutokana na makubaliano ya juu, mgombea pekee wa Urais wa CAF Patrice Motsepe tayari anatoka Anglophone [maana yake anaingia moja kwa moja kwenye baraza wajumbe wa FIFA] kwa hiyo inabaki nafasi moja, wagombea tulikuwa sita, katika hao sita mmoja anatoka kwenye ukanda wetu [CECAFA].
“Jana tulikuwa na kikao chetu cha CECAFA tukakubaliana kwa sababu mimi ni kiongozi wa zone tukakubaliana kumwachia mwenzangu wa Kenya Nick Mwendwa.”