WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kushikamana, kudumisha amani na wapuuze kauli za chuki zinazotolewa na watu wasioitakia mema nchi kuhusu afya ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwani ni mzima wa afya.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Machi 12, 2021) baada ya kushiriki sala ya Ijumaa mjini Njombe, ambapo amesisitiza kuwa Rais anafanya kazi kulingana na mpango kazi wake. Amesema wananchi wanatakiwa kushikamana na kuifanya nchi kuendelea kuwa na amani na utulivu.
Bonyeza Play kusikiliza alichozungumza Waziri Mkuu Majaliwa
RC CHALAMILA ASEMA RAIS MAGUFULI YUKO IMARA “NIMEONGEA NA JPM LEO”