Tanzania imepata Rais wa kwanza Mwanamke ambae ni Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambae amechukua nafasi hiyo kufuatia kifo cha aliyekua Rais wa Tanzania Hayati Dr. John Pombe Magufuli, kitendo cha Rais Samia kuketi kwenye kiti hicho kimeleta pongezi nyingi na hata Wanawake wengi kunyanyuka na kuzungumza jambo.
Mmoja wa walioandika ni Mwigizaji maarufu wa Tanzania Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa ambae ameandika –> “Hatuwezi kuwa sawa na Wanaume haswa kimaumbile lakini tunaweza kuwa sawa nao kimawazo na mtazamo wa kiuongozi kujenga nchi, watabaki Wanaume tutabaki Wanawake, wataitwa Baba na sisi Mama, tufundishane namna ya kuishi kwa upendo na hii iende hadi kwa watoto wetu”
Tukiachia mbali hii ya Monalisa, pongezi za Tanzania kuwa na Rais wa kwanza Mwanamke zilimiminika kutoka sehemu mbalimbali duniani ikiwemo kutoka kwa Makamu wa sasa wa Rais wa Marekani Kamala Harris ambae aliandika kumtakia kila la kheri Rais Samia na kusema Marekani ipo tayari kufanya kazi nae kuimarisha uhusiano kati ya Nchi hizo mbili.
Mwingine ambae alimpongeza Rais Samia ni Hillary Clinton ambae ni Mke wa Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton lakini pia Hillary alikua Mgombe Urais wa Marekani mwaka 2016 akichuana na Donald Trump, Hillary aliandika “kila la kheri kwa Samia Suluhu, Rais mpya wa Tanzania na Mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Tanzania”
LIVE: RAIS SAMIA AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU MAMLAKA YA BANDARI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA