Spika, wa Bunge, Job Ndugai amewataka mawaziri kuzingatia ushauri wanaopewa na wabunge ambao wamekuwa wakibeba mawazo mengi ya wananchi.
Ndugai amebainisha hayo leo Alhamisi bungeni Jijini Dodoma na kusema kuwa kwa nafasi walizokuwa nazo kama mawaziri watapata ushauri wa kutosha kutoka serikalini lakini itakuwa vizuri kuchukua ushauri wa wabunge.
“Kwahiyo tusisahauliane sana mtapata ushauri mwingi sana kutoka huko Serikalini lakini msisahau ushauri wa wabunge ni ushauri muhimu sana kwasababu ni ushauri wa wananchi utakaowasaidia kushughulikia mambo fulani fulani ya msingi katika Wizara zenu” Ndugai.
“Kwa mfano mimi kila siku nasikia habari za wafanyabiashara wa nchi hii wakilalamika hivi Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara na Fedha hiyo kada ya biashara mnahitaji kengele gani igongwe kusema hili eneo ni kipaumbele namba moja” Spika Job Ndugai.
“Yapo mambo mengi sana ya kufanya kila mmoja katika wizara yake na mengi sana mtayapata kama ushauri kutoka kwa waheshimiwa wabunge cha msingi waheshimiwa mawaziri nyinyi ni wabunge kama sisi hilo ndilo la msingi hapa bungeni ndio nyumbani huko mmeenda matembezi tu” Spika Ndugai
“Kwahiyo tusisahauliane sana mtapata ushauri mwingi sana huko serikalini lakini msisahau ushauri wa wabunge ni ushauri muhimu sana kwasababu ni ushauri wa wananchi kabisa kabisa na kila wizara ina mambo fulani fulani ya msingi ya kushughulikia” Job Ndugai, Spika wa Bunge
“Sisi kama wabunge tunamshukuru sana rais wetu mpendwa tukiamini kwamba dhamana hii waheshimiwa mawaziri mmeipata mtaifanyia kazi kwa imani ile ile mheshimiwa rais aliyowapatia” Spika, Job Ndugai
“Niwapongeze sana mawaziri wetu na manaibu wao kwanza kwa kubaki kwenye baraza na huo ndio uzuri wa mama amekuwa ‘very considerate’ (Umakini wa kutowaumiza wengine) na huo ndio ukweli wangekuwa wenzetu wengine upewe panga hilo majeruhi yangekuwa kibao lakini mama kapita salama katikati,”- Spika, Job Ndugai.