Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewataka mawaziri, manaibu wao na wabunge wote wawepo bungeni kesho Alhamisi Aprili 22, 2021 wakati Rais wa awamu ya sita, Samia Suluhu Hassan atakapolihutubia Bunge.
Rais Samia aliyeapishwa Machi 19, 2021 baada ya kifo cha rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021 kesho atalihutubia Bunge kwa mara ya kwanza tangu awe kiongozi mkuu wa nchi.
Akizungumza leo “Kesho tutakuwa na ugeni mkubwa sana hapa Rais wa awamu ya sita anakuja kulihutubia Bunge. Huwezi kujua kesho wala kesho kutwa, si vizuri kutokuwepo kwenye landmark ya mheshimiwa Rais wa awamu wa sita anapokuja kulihutubia Bunge hili.”
“Wale mawaziri na manaibu ambao wako huko sijui wapi wote wawepo kesho. Warudi wote wawepo kesho. Ukumbi utakuwa umejaa wote, gallery zote halafu ndani ya ukumbi wa bunge….haitaeleweka,” Ndugai
DC SABAYA AKUTA MAFUTA LITA TANO YANAUZWA ELFU 34, AKASIRIKA AMBANA MFANYABIASHARA “TUTAZINGUANA”