Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Pwani, Mhandisi Yudas Msangi, amesema Daraja jipya la Wami lenye urefu wa mita 510 na Barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 3.8 linalounganisha miji ya Chalinze – Pwani na Segera – Tanga litakamilika mwezi Septemba mwaka huu.
Mhandisi Msangi amemueleza Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, mkoani Pwani wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi huo uliofikia 50.5% na kumuahidi kuwa kazi itakamilika kama ilivyopangwa.
Naibu Waziri Waitara amesema ujenzi wa Daraja jipya la Wami ni mkakati wa Serikali katika kuongeza ufanisi katika barabara ya Chalinze – Segera na kupunguza adha kwa abiria na wasafirishaji wanaotumia daraja la zamani lenye urefu wa mita 88.75.
“Kutokana na umuhimu wa daraja hili Serikali imeamua kujenga daraja jipya ili kuondoa adha katika daraja la zamani lililojengwa mwaka 1959 kutokana na kutokidhi mahitaji ya magari yanayopita kwa sasa, kuwa jembamba na lenye njia moja na Barabara zake unganishi kupita katika miinuko mikali na kona mbaya na hivyo kusababisha ajali za mara kwa mara”———Waitara
KIJANA ALIEANZA KUPAKA RANGI HADI KUMILIKI KAMPUNI NA KUAJIRI “NILIACHA MZIKI, NKAWA FUNDI TILES”