Katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni Mbunge wa viti maalumu, Felister Njau amesimama na kuuliza swali akitaka kujua mikakati ya Serikali katika kutatua tatizo la mafuriko katika maeneo ya Mbweni Teta, Bunju Basihaya, Kunduchi, Nyamachabes. Ununio na Mikocheni katika jimbo la Kawe.
Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, David Silinde amejibu na kusema kuwa Serikali imetenga BILIONI 8.4 kwa ajili ya Ujenzi wa Mifereji wa maji ya mvua katika kata ya Mbweni ili kuondoa kero ya mafuriko.
MBUNGE ACHARUKA UBAMBIKIZAJI KESI ZA UHUJUMU UCHUMI AMWAMBIA WAZIRI JARIBU KULALA GEREZANI SIKU MOJA