Kwa mwaka wa pili mfululizo, Tanzania imetajwa tena kuwa ni Nchi ya kwanza Afrika Mashariki ambayo bei ya bando zake za Internet ni nafuu kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na Mtandao wa Utafiti wa Cable wa nchini Uingereza.
Kwenye ripoti hiyo yenye Takwimu za Dunia nzima ambazo zimekusanywa kuanzia December 08,2020 hadi February 25,2021 inaonesha kuwa Tanzania ina Bando rahisi ambayo ni USD 0.75 (Tsh. 1,742.81) kwa GB moja ikifuatiwa na Rwanda (USD 1.25), Uganda (USD 1.56) na Burundi (USD 2.10).
Kenya ilikuwa ya pili mwaka jana ambapo bando iligharimu USD 1.04 kwa kila GB lakini kwa mwaka huu gharama zimepanda na kufikia USD 2.25.
ULIPITWA? RC CHALAMILA ASEMA WANAFUNZI WALE WACHAPWE VIBOKO, SHULE CHINI YA ULINZI MIEZI 6