Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu 161 wanaotuhumiwa kujihusisha na wizi wa pikipiki, magari na vifaa vyake.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni matokeo ya operesheni iliyofanywa na polisi kuanzia Aprili 20, 2021 baada ya kuwepo kwa malalamiko ya wamiliki wa vyombo hivyo vya moto kutoka maeneo mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Mei 6, 2021 na kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema wamefanikiwa kuwakamata vinara watano wa wizi huo.