Sakata la wafanyabiashara wawili , William Taitas Mollel na Dkt Philemon Mollel (Monaban)wakazi wa jiji la Arusha kutishiana kuuwana kwa silaha katika ugomvi wa kugombea eneo lililoamuriwa na mahakama, limechukua sura mpya Mara baada ya wafanyabiashara hao kuitwa mahakamani kuu .
Mbele ya jaji Abdalah Gwae wa mahakama kuu Kanda ya Arusha aliwataka wafanyabiashara hao kutihatarisha amani ya nchi na wazingatie maamuzi yaliyotolewa na mahakama.
Kwa mujibu maamuzi yaliyotolewa Mei 7 ,2021 na Jaji mfawidhi kanda ya Arusha ,Jaji Moses Mzuna alitamka kwamba Mollel ni mvamizi wa eneo la marehemu Titus Aaron Mollel lililoko Ngulelo jijini Arusha na hivyo kutakiwa kuondoka kwenye eneo hilo lenye ukubwa wa hekari saba .
Hata hivyo jaji Gwae Mara baada ya kusikiliza madai ya pande zote mbili kwa niaba ya Jaji Mfawidhi Moses Mzuna aliwafahamisha pande zote kutumia busara na kutohatarisha amani kwa kuwa Jambo hilo lilishaamuliwa na mahakama.