Emmanuel Cosmas ni kijana mwenye umri wa miaka 18 ambapo akiwa na miaka 11 aliweza kubuni kifaa cha ulinzi ambacho kinaweza kutumika sehemu mbalimbali ikiwemo manyumbani na kinaweza kuonyesha ishara endapo kitakanyagwa.
Cosmas anasema amekuwa akifanya shughuli mbalimbali ambapo alishindanishwa kwenye mataifa 191 katika mashindano ya ubunifu na aliweza kuwa mshindi kati ya watu watano ambapo alichaguliwa kuwa msemaji au balozi wa UNICEF kwa upande wa vijana nchini Tanzania katika sekta ya ubunifu na maji safi na salama.
“Mikeka hii ninayotengeneza ni salama unaweza kuweka mlangoni mtu akiukanyaga una sense na nimetengeneza kwa plastiki,mwaka jana nilishindanishwa kwenye mataifa 191 kwenye mashindano ya ubunifu ambapo nilichaguliwa kuwa balozi wa shirika la watoto duniani UNICEF”-Emmanueli
WAFANYABIASHARA ARUSHA WARUSHIANA RISASI, MAHAKAMA YAWAITA “POLISI WALINDE”