Watu wanne wa Kijiji cha Nguyami Kata Idibo Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro wanaashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufukua kaburi la marehemu aliyefahamika kwa jina la Rehema Michel.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kuripotiwa kwa tukio la kufukuliwa kaburi la Marehemu huyo ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Fortunatus Muslim amewataka wananchi kutoa ushirikino kwa Jeshi hilo ili kuwabaini wahusika walioshiriki katika kitendo hicho.