Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Dk Damas Ndumbaro amemsimamisha kazi meneja msitu wa Mkoa wa Geita, Tadeus Shirima ili kupisha uchunguzi.
Dk Ndumbaro amemwagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silay kupeleka mtu mwingine Geita.
Shirima amesimamishwa kufuatia operesheni aliyoendesha katika Wilaya ya Bukombe inayodaiwa haikuwa na kibali cha viongozi wake.
Waziri Ndumbaro amesema walipokea malalamiko kutoka kwa mbunge wa Bukombe kuhusu operesheni hiyo iliyosababisha hasara kwa wananchi.