Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya M. Kikwete akiwa kwenye mradi wa kufua umeme kwa njia ya maji wa megawati 2115 wa Julius Nyerere aliipongeza Serikali ya awamu ya tano iliyokuwa chini ya Hayati Dkt. John Magufuli kwa kuonesha uthubutu wake kwa kuanzisha ujenzi wa mradi huo ambapo alishauri Wizara ya Nishati kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwa fursa zitakazo ambatana na kukamilika kwa bwawa hilo.
Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuwa, mradi wa Julius Nyerere utakapokamilika utakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa sambamba na kuchochea ukuwaji wa uchumi wa Taifa zima kwa ujumla.
“Nina uhakika Rais Samia Suhulu Hassan, atahakikisha mradi huu unakwenda sambamba na matarajio ya mtangulizi wake na kukamilika kwa wakati” Dkt. Kikwete.
Aliongeza kuwa, wananchi wa Mikoa kumi na moja, iliyo na vyanzo vya maji ya mto Rufiji ambao unategemewa sana katika bwawa la Nyerere kuvilinda vyanzo hivyo kwani bila kuvilinda mradi huo hautaleta tija.