Ni Headlines za Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt Hamis Kigwangalla siku kadhaa zilizopita aliwahi kutangaza kwamba ameshajipata chanjo ya kinga ya Ugonjwa wa Corona (Covid-19).
Sasa leo July 26, 2021 anazimiliki vichwa vya habari baada ya kuipinga kauli ya Mbunge wa Kawe Askofu Gwajima aliyoitoa jana katika Kanisa lake akiwataka watanzania kupuuzia chanjo hizo.
Kigwangalla aliandika…“Binafsi niliwahi kuwa na msimamo wa kukataa chanjo na niliuweka wazi. Nilipopata taarifa mpya na sahihi nilikimbia kuweka wazi mabadiliko ya msimamo wangu, haswa nikihofia watu kukataa chanjo kwa kuwa tu mtu mmojawapo mwenye ushawishi kwenye jamii kakataa chanjo”– Mbunge wa Nzega Vijijini, Hamisi Kigwangalla
“Tumerithi nchi yenye kuruhusu mijadala, ndiyo maana Askofu Gwajima anatumia haki yake ya kusema lakini ukiwa na maadili kidogo tu na ukajua nafasi yako kwenye jamii, utajitenga na uongo na kusimama na ukweli, kwa sasa utajua ukiwa una ushawishi basi utashawishi watu vibaya”– Hamis Kigwangalla
“Askofu Gwajima afanye uungwana azitafute makala za kisayansi asome kwa kina juu ya chanjo; na kama ana mashaka na sayansi yake atafute wataalamu wampe shule ya chanjo. Hata mimi Mbunge mwenzake nimesoma soma kidogo, niko tayari kumfafanulia maeneo kadhaa na kumuondoa shaka”- Hamis Kigwangalla
“Kwenye dunia ya sayansi na usomi, Kama ilivyo kwenye maisha ya kawaida, watu hubadili misimamo kutokana na kupata taarifa mpya, na sahihi zaidi; na ndiyo maana kila siku tunafanya tafiti na kujifunza, na kuboresha. Ndiyo maana leo kuna iPhone 12! misimamo haiwagi kama jiwe”– Hamis Kigwangalla
“Kama ambavyo mimi nilibadili msimamo wangu juu ya Chanjo baada ya ujio wa taarifa mpya za kisayansi juu ya usalama na uwezo wa chanjo, ndivyo ninaamini hata kaka yangu Askofu Gwajima atabadili msimamo wake na kujiunga na serikali kuhamasisha tutumie chanjo kujikinga” —Hamisi Kigwangalla.
KIGWANGALLA AMLIPUA GWAJIMA KUHUSU CHANJO ASEMA ‘ATAFUTE WATAALAMU WAMPE SHULE’