Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kenan Kihongosi amekishauri chama chake kiwashughulikie wale wote wanaoendana kinyume na maelekezo ya chama hicho wakiwepo viongozi wake.
Kihongosi ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari ambapo pia amewataka Watanzania kuweza kujitokeza kuchoma chanjo ya Corona iliyowasili hivi karibuni.
Kauli ya Katibu Mkuu huyo inakuja ikiwa ni siku mbili toka Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe kupitia CCM kuweka wazi msimamo wake wa kukataa chanjo dhidi ya Corona.
“Msimamo wa Serikali ni kulinda Wananchi na chanjo itakapotolewa kwa Wananchi, Chanjo itawapa nafuu ya kujikinga dhidi ya maradhi ya Corona lakini anapotokea Kiongozi mmoja wa muhimili na kuhamasisha watu na kutuma ujumbe kwamba chanjo hazifai na zinamadhara”-Kihongosi
“NI utovu wa nidhamu maana chama kina taratibu zake na kama kuna Mbunge anahoja kuna namna ya kuwasilisha hoja zake kwenye chama. Sisi umoja wa Vijana wa CCM kauli zile tunazilaani na tuzipinga vikali.” Amesema Kihongosi.
“Tumuhoji yeye ni daktari amesomea basi atume majibu kwahiyo sisi UVCCM kauli zile tunazilaani na kuzipinga kikali utaratbu wa Mbunge anapokuwa na hoja basi lazima alete sehemu husika na wala si kupeleka kwenye Umma”-Kihongosi
KIGWANGALLA AMLIPUA GWAJIMA KUHUSU CHANJO ASEMA “ATAFUTE WATAALAMU WAMPE SHULE”