Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imetoa Ripoti yake leo Bungeni Dodoma kuhusu shauri la Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima baada ya kumaliza kumuhoji kwa tuhuma za kuzungumza uongo na kulishushia Bunge hadhi.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo akisoma taarifa yake amesema Shahidi alikiri kauli zote ni zake 100% na akasema ni mahubiri ———> “niliyasema nikiwa Kanisani na ninayasema kama Askofu, kosa kubwa ni kujaribu kuyakosoa mahubiri, huwezi ku-question mahubiri, Kamati ilijiridhisha kuwa mahubiri yanayotolewa yanapaswa kuzingatia Sheria za Nchi hivyo kauli zinazotolewa haziwezi kuwa na kinga ya kuhojiwa”
“Gwajima ni Mbunge na Kiongozi kwa hiyo anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa, tuhuma za kuchonganisha Mhimili wa Bunge na Serikali au Serikali na Wananchi zinajidhihirisha wazi kwenye kauli za Askofu Gwajima”
“Gwajima alishindwa kuthibitisha kauli zake na hana kielelezo chochote kama alivyowaaminisha Wananchi, suala la Viongozi kupewa rushwa hakutoa ushahidi wowote, kamati imemtia hatiani Askofu Gwajima”
“Kuhusu adhabu ya utovu wa nidhamu uliokithiri wa Askofu Gwajima ni kuwa kanuni zinataka asihudhurie mfululizo mikutano miwili au isiyopungua mitatu, Kamati ilishangazwa na vitendo alivyovifanya mbele yake na iliona ni dharau”
“Askofu Gwajima hakukiri wala kujutia makosa yake, alionyesha dharau hivyo Kamati imemtia hatiani, Bunge linaazimia kuwa apewe adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili mfululizo ya Bunge baada ya kupitisha azimio hili” ——— Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maadili Emmanuel Mwakasaka.