Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake wameomba wasisomewe mashitaka yanayowakabili katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu kutokana na madai kwamba hati ya mashitaka ina mkanganyiko.
Hatua hiyo inakuja baada ya Mahakama hiyo mbele ya Jaji Elineza Luvanda kutupilia mbali pingamizi la washitakiwa hao la kutaka kuachiwa huru katika kesi ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi ambalo waliwasilisha August 31, 2021 kupitia Wakili Peter Kibatala.
Miongoni mwa hoja mpya za leo tatu wamedai kwamba hati ya mashitaka haijaeleza kama wana nia ya kufanya ugaidi, kujirudia kwa makosa katika hati ya mashitaka na makosa ya ugaidi hayawezi kuchanganywa na ya kula njama.
Kesi imeahirishwa hadi Septemba 3, 2021 kwa ajili ya mahakama kutoa uamuzi baada ya Upande wa Mashitaka kuomba muda kuwasilisha majibu yao.
TAZAMA KILICHOIJIRI LEO KATIKA KESI YA MBOWE MAHAKAMA YA MAFISADI