Siku chache tangu kuuawa kwa Hamza na polisi August 25, 2021 baada ya kuwaua kwa risasi Askari watatu na Mlinzi mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amezungumza leo Mkoani Mwanza na kusema uchunguzi uliyofanywa na Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa Gaidi wa kujitoa mhanga.
“Uchunguzi wetu uligusa mambo matatu, kwanza tulitaka kujua Hamza Mohammed ni nani, nini kilimsukuma Hamza kwenda kufanya tukio lile na kutaka kutambua mshiriki mwingine katika tukio hilo”- DCI Wambura
Ayo TV & Millardayo.com imekusogezea taarifa kamili hapa unaweza ukabonyeza play kufahamu kilichosema na DCI Wambura kuhusu Hamza.