Ripoti kutoka nchini Guinea zinaarifu kuwa hatma ya Rais wa Nchi hiyo Alpha Condé haijulikani baada ya video ambayo haijathibitishwa kumuonesha akiwa mikononi mwa Wanajeshi, ambao wamehutubia Taifa hilo na kusemwa wamefanya mapinduzi.
Ikiwa ni siku kadhaa tangu Wanajeshi wa Guinea wamejitokeza katika runinga ya taifa wakithibitisha kwamba Rais Alpha Conde ameondolewa madarakani, katika hotuba iliyooneshwa kwenye televisheni, Wanaume waliovaa sare za kijeshi, bendera ya Guinea ikiwa nyuma yao wamelihutubia taifa wakijiita Kamati ya Kitaifa ya upatanisho na maendeleo.
Sasa mengine yaliyoibuka ni kwamba baada ya kuonekana kwa kamanda aliehutubia taifa hilo kumbe aliwahi kuwa msaidizi wa Rais huyo.