Ndege inayofahamika kwa jina la Edelweiss kutokea nchini Switzeland imetua nchini Tanzania ikiwa na watalii 270 ambapo itakuwa ikifanya safari zake nakutua katika Uwanja wa KIA na Zanzibar.
Waziri wa maliasili na Utalii Dkt Damasi Ndumbaro,Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mabarawa, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa na viongozi wengine wameshiriki katika mapokezi ya ndege hiyo.
“Tunaipokea ndege hii kwa mara ya kwanza ikiwa na watalii 270 ujio wao unaonyesha nchi yetu ni salama kutokana na hatua alizozichukua Rais mama yetu Samia Hassan katika kupangana na janga la uviko 19”-Dkt Damas Ndumbaro Waziri wa maliasili na Utalii.
“Wana ndege zaidi ya 270 tutarajie ndege nyingi kutoka ulaya zitakuja na hii inatokana na kazi kubwa iliyofanywa na nchi yetu,Tanzania ni salama watanzania wanachanjwa”-Gerson Msigwa Msemaji Mkuu wa Serikali.
TAZAMA NDEGE MBILI MPYA AIRBUS ZILIVYOTUA ZANZIBAR ZIKITOKEA CANADA, RAIS MWINYI AZIPOKEA