Baada ya thamani ya kampuni ya Tesla kupanda na kufikisha thamani zaidi ya Dola Trilioni 1; wiki hii CEO wa Tesla – Elon Musk anayemiliki 23% ya hisa za kampuni ya Tesla; alifikisha utajiri wa Dola Bilioni 271.3, katika mtandao wa Forbes. Ni kiasi kikubwa ambacho hakijawahi kurekodiwa na Forbes tangu ilipoanzishwa mwaka 1982.
Elon amekuwa tajiri wa kwanza kufikisha umiliki wa fedha nyingi katika historia ya Forbes. Jeff Bezo alikuwa na rekodi kubwa kwa kuwa na umiliki wa Dola Bilioni 212 (Tshs Trilioni 489). Elon wiki hii alifikisha utajiri wa Bilioni 271.3 (Tshs Trilioni 625) na kuweka rekodi kubwa ambayo hajawahi kuweka tajiri yoyote katika historia ya Forbes.
Hivi karibuni Jeff amerudi nafasi ya kwanza kwa kuwa na umiliki wa Dola Bilioni 201 (Tshs 463), na Elon ameshuka nafasi ya pili kwa kumiliki Dola Bilioni 190.5 (439).