Mahakama ya Sudan imeamuru kurejeshwa mara moja kwa huduma za mtandao wa intaneti zilizokatwa wakati wa mapinduzi ya kijeshi zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Kwa mujibu wa Wakili Abdelazim Hassan aliyezungumza na Shirika la Habari la AFP, Mahakama ya Wilaya Mjini Khartoum imeamuru huduma za intaneti kurejeshwa mara moja. Kiongozi wa Sudan akutana na ujumbe wa Nchi za Kiarabu
Hata baada ya agizo la Mahakama, nchi imesalia bila ya mtandao wa intaneti mapema siku ya Jumanne. Kesi hiyo ilifunguliwa na kundi la wanasheria na jumuiya ya ulinzi wa wateja wa Sudan.
Mahakama pia imeamuru huduma ziendelee kutolewa hata wakati wa mchakato wa rufaa.
Upatikanaji wa intaneti nchini Sudan kwa kiasi kikubwa ulizuiwa tangu Oktoba 25, siku yalipofanyika mapinduzi ya kijeshi yaliyolaaniwa na watu wengi, huku mawasiliano ya simu pia yakitatizika mara kwa mara.