Inaelezwa kwamba wakiwa Doha, Qatar October 2020 Wanawake hao wanadai waliambiwa washuke kwenye ndege yao ya Qatar Airways na kulazimishwa kukaguliwa bila ridhaa yao bika kupewa maelezo ya wazi ni nini kinaendelea ambapo yote hiyo iligundulika ilikua ni msako wa kumtafuta Mama wa Mtoto huyo mchanga aliyekutwa kwenye mfuko wa plastiki ndani/kando ya pipa la taka kwenye moja ya vyoo vya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad.
Kufuatia kupatikana kwa Mtoto huyo mchanga, zaidi ya Wanawake 18 kutoka kwenye ndege 10 tofauti wakiwemo raia 13 wa Australia waliokuwa kwenye ndege inayoelekea Sydney walihusishwa kwenye vipimo hivyo baada ya kutolewa ndani ya Ndege na Askari wa Qatar wenye silaha na kufanyiwa uchunguzi wa kimwili kwenye Ambulance ya uwanja wa ndege.