Idadi ya Watu wanaofariki kutokana na matumizi ya mihadarati imevuka laki moja kwa mwaka nchini Marekani, Wataalamu nchini humo wamesema vifo hivyo vimetokana na matumizi zaidi ya mhadarati unaoitwa Fentanyl.
Idara Kuu ya kudhibiti magonjwa ya Marekani (CDC) imetoa taarifa hiyo na kueleza kwamba Watu wengi zaidi wanafariki kwa mwaka kutokana na matumizi ya dawa za kulevya kuliko wale wanaofariki kutokana na kupigwa risasi au na ajali za barabarani.
Idara hiyo imesema matumizi ya mihadarati yameongezeka kwa asilimia 28.5 kati ya mwezi Mei mwaka 2020 hadi mwezi Aprili mwaka huu wa 2021.
Mkurugenzi wa Kitaifa wa Kudhibiti Sera ya Dawa za Kulevya nchini Marekani Dr. Rahul Gupta amesema hali hii isiyo ya kawaida haikubaliki na inahitaji kutafutatiwa majibu ya haraka.