Watu watano wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi wameuawa na Polisi Mkoani Kigoma katika Ziwa Tanganyika baada ya kupora vifaa mbalimbali vya uvuvi usiku wa kuamkia leo ambavyo ni pamoja na mashine tatu za boti, simu za wavuvi pamoja na nyavu za kuvulia.
“Vitendo vya utekaji kwa njia ya barabara sasa vimedhibitiwa lakini Majambazi wamejipeleka kwenye maji, sisi Polisi Nchi kavu tupo na majini tupo ni bora sasa Watu wakabadili maisha kwa kufanya kazi halali kuliko kushiriki kwenye vitendo vya kihalifu, na hii ni salamu tu kwamba hatulali waache ujambazi” ——— RPC Kigoma, James Manyama
Kamanda Manyama amesema Majambazi wawili wamefariki kwenye msako huo ndani ya maji huku wengine watatu wakitokomea katika Ziwa Tanganyika baada ya kupigwa risasi na kujirusha ndani ya maji, Polisi wanaendelea kuwasaka na pia kutafuta miili ya waliozama.