Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeandaa mafunzo kwa wadau wa nyaya za umeme wanaojishughulisha na utengenezaji, uagizaji, usambazaji uuzaji na watumiaji wa nyaya za umeme katika mkoa wa DSM ili kuhakikisha wanatengeneza nyaya ambazo zinakidhi viwango na ubora unaotakiwa.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), David Ndibalema amesema ikiwa mtumiaji hawezi kupata nyaya za umeme zenye ubora itasababisha kuwepo kwa malalamiko juu ya thamani ya maisha yao na fedha zao.
Amesema mafunzo hayo yanalenga kuwashirikisha washiriki ili wawe kwenye muelekeo mzuri zaidi katika kutekeleza matakwa ya viwango husika pamoja na huduma wanazotoa kwa jamii.
“Warsha hii imewalenga wadau wa makundi wasiopungua 30 kutoka mkoa wa Dar es Salaam na kwa hadhara hii napenda kusema kwamba tumetiwa moyo sana kwa mwitiko wa mwaliko wetu mliouonesha”. Amesema
Aidha amesema wataendelea kushirikiana na wadau wa nyaya za umeme nchini ili kuhakikisha wanaweza kuzalisha nyaya zenye ubora unaotakiwa kwa watumiaji wa nyaya za umeme.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.David Ndibalema akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wadau wa nyaya za umeme wanaojishughulisha na utengenezaji, uagizaji, usambazaji uuzaji na watumiaji wa nyaya za umeme katika Mkoa wa Dar es Salaam. Meneja wa Mafunzo na Utafiti TBS, Bw.Hamisi Mwanasala akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wadau wa nyaya za umeme wanaojishughulisha na utengenezaji, uagizaji, usambazaji uuzaji na watumiaji wa nyaya za umeme katika Mkoa wa Dar es Salaam. Kaimu Meneja Viwango TBS Bi.Nasra Yusuf akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wadau wa nyaya za umeme wanaojishughulisha na utengenezaji, uagizaji, usambazaji uuzaji na watumiaji wa nyaya za umeme katika Mkoa wa Dar es Salaam.Wadau wa nyaya za umeme wanaojishughulisha na utengenezaji, uagizaji, usambazaji uuzaji na watumiaji wa nyaya za umeme katika mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa na TBS kwaajili ya kuwajengea uwezo waweze kutengeneza, kuuza, na kusambaza nyaya za umeme zilizokidhi viwango