Mahakama ya Juu Nchini humo imetupilia mbali ombi la Chama Kikuu cha Upinzani la kubatilisha matokeo ya Uchaguzi wa Rais wa Desemba 4, ambapo Rais Adama Barrow alitangazwa mshindi
Kiongozi wa Chama cha United Democratic Party (UDP), Ousainou Darboe aliyepata 28% ya Kura alisema Kampeni za Uchaguzi zilihusisha rushwa
Chama hicho kilidai Barrow au Wanachama wa Chama chake cha National People’s Party walikuwa wanatoa fedha au zawadi kwa Wanakijiji ili wapate kura.