Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amefanya uteuzi maalumu wa wajumbe 12 wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Serengeti Music Festival.
Tamasha hilo maalumu linaandaliwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wizara ya Sanaa, kwa ajili ya kuziunga mkono jitihada za wasanii wa muziki wa nchini ikiwa ni pamoja na kuinadi sekta ya utalii kwa kuwaleta pamoja na kutoa burudani kwa mashabiki wao katika maeneo mbalimbali ambayo Tamasha hilo litapita.
Miongoni mwa wajumbe walioteuliwa ni pamoja na watangazaji mahiri wa vipindi vya burudani Bdozen , Mammybaby pamoja na Lillommy.