Mshambuliaji wa Chelsea FC, Romelu Lukaku ameomba radhi kwa kocha wake Thomas Tuchel pamoja na mashabiki wa mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, ikiwa siku kadhaa baada ya mahojiano ya dhihaka kwa kocha wake aliyofanya na Sky Sports kuwekwa hadhari kituo hicho.
Lukaku ameomba msamaha baada ya kuonesha hisia zake chanya juu ya mbinu za kocha wake zinazombelekea Mbelgiji huyo kukosa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara ambapo Kai Havertz amekuwa akitumika mara nyingi kama namba tisa.
Kufuatia mazungumzo ya Lukaku na kocha wake Tuchel , mchezaji atazamiwa kulipa faini ya Euro Laki sita sawa sawa na Billion 1.5 za kitanzania ikiwa kama adhabu ya kuvunja sheria za matumizi ya viombo vya habari za klabu ya Chelsea pamoja na kukomesha tabia hiyo ya kumzungumzia kocha wake vibaya.
Lukaku aliachwa nje ya kikosi cha Chelsea walipocheza dhidi ya Liverpool kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya 2-2.