Gari la Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mwanza lililokuwa kwenye ziara ya RC wa Mwanza limepata ajali eneo la Busega likiwa linaelekea Ukerewe kupitia Bunda.
Miongoni mwa viongozi walioguswa na ajali hiyo ni Waziri wa Habari, Nape Nahuye ambae kupitia ukurasa wake wa twitter ameyaandika haya.
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya gari iliyosababisha vifo vya Maafisa Habari, Waandishi wa Habari wa Mwanza na Wananchi”- Waziri Nape
“Natoa pole kwa Familia za Marehemu, Waandishi wa Habari wote, ndugu, jamaa na marafiki.Mungu aziweke mahali pema roho za marehemu wote, Amina”- Waziri Nape