Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa limesema zaidi ya nusu ya watu wote barani Ulaya wanatazamiwa kuwa wataambukizwa kirusi cha corona aina ya Omicron katika muda wa miezi miwili inayokuja.
Mkuu wa WHO kanda ya Ulaya Hans Kluge amesema tathmini hiyo ni kwa mujibu wa taasisi ya takwimu za afya ya IHME na imetolewa wakati kirusi cha omicron kinaendelea kusambaa kwa kasi duniani.
Bara la Ulaya limekuwa kitovu cha idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona hali iliyopelekea serikali nyingi kutangaza vizuizi vipya na kutanua kampeni ya utoaji chanjo za nyongeza dhidi ya Covid-19.
WHO imesema ingawa kirusi cha omicron kinasambaa haraka ikilinganishwa na aina nyingine zilizotangulia, chanjo zilizoidhinishwa bado zinaweza kutoa kinga dhidi ya watu kupata maradhi makali na hata kifo.
Via DW Swahili