Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson leo atahojiwa kuhusiana na sherehe zilizofanywa na wafanyakazi wa ofisi yake kipindi ambapo nchi ilikuwa kwenye vikwazo na sheria kali katika kuzuia usambaaji wa virusi vya corona.
Sherehe hizo ambazo zilifanyika katikati na mwishoni mwa mwaka 2020 zimezua mjadala mkubwa mpaka kupelekea wabunge na wapiga kura wengi kumtaka Waziri Mkuu huyo ajiuzulu.
Picha kadhaa zilisambaa mitandaoni zikimuonyesha Waziri Mkuu akiwemo kwenye sherehe hizo, pamoja na mashuhuda wengine kutoa ushahidi ambao umesababisha Waziri Mkuu aitwe na kuhojiwa.
Mahojiano hayo yatarushwa moja kwa moja kupitia stesheni za habari nchini Uingereza na mitandaoni.