Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imemkuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake 6 kwenye kesi ya uhujumu uchumi ambapo Hakimu Dkt Patricia Kisinda amesema Mahakama imepitia vielelezo 12 pamoja na mashahidi 13 walioletwa na upande wa jamhuri katika kuthibitisha mashtaka yanayowakabili Washitakiwa ambapo imewakuta na kesi ya kujibu.
Akiongea kwa niaba ya Washtakiwa wote, Wakili wa upande wa utetezi wakili Moses Mahuna amesema watakuwa na Mashahidi wasiopungua kumi na watajitetea chini ya kiapo.
Lengai Ole Sabaya na wenzake sita wanatuhumiwa kuchukua fedha shilingi milioni 90 kutoka kwa Mfanyabiashara Francis Mroso kwa madai kwamba amekwepa kodi.
Watuhumiwa katika kesi hiyo ni lengai ole sabaya,Silvesta Nyegu,Enock Togolane Mkeni,Watson Mahomange,John Odemba,Nathan Msuya na Jackson Macha.
SABAYA ATOA CHOZI, AOMBA AACHIWE HURU “WALITAKA KUNIUA, KESI IMETENGENEZWA”
KAZI ZA VIJANA WA SABAYA ZATAJWA,GARI YAKE YAONYESHWA TENA