Rais wa Mali aliyeondolewa madarakani Ibrahim Boubacr Keita amefariki akiwa na umri wa miaka 76 , familia yake na rafiki zake wamesema.
Miaka miwili iliopita aliugua kiharusi lakini chanzo cha kifo chake siku ya Jumapili hakikuwekwa wazi.
Alifariki mwendo wa saa tatu saa za Uingereza nyumbani kwake mjini Bamako , mmoja wa ndugu zake alikiambia chombo cha Habari cha AFP.
Keita aliiongoza Mali kwa miaka saba hadi 2020, wakati alipopinduliwa baada ya maandamano makubwa dhidi ya serikali kutokana na jinsi alivyolishughulikia suala la Wanajihad.
Mgogoro wa kiuchumi na uchaguzi ulio huru pia ulisababisha maandamano hayo dhidi ya utawala wake.