Greyson Mahembe ambaye ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi alijinyonga kwa tambala la kudekia akiwa Mahabusu ya kituo cha Polisi Wilaya ya Mtwara, Mkoani Mtwara.
Greyson alikuwa miongoni mwa Maofisa wengine wa Polisi saba wanaotuhumiwa kuumua kijana Musa Hamisi (25) ambaye ameuawa baada ya kudai fedha zake shilingi Milioni 33.7 ambazo Maafisa hao wanadaiwa kuzichukua kutoka kwa kijana huyo baada ya kumfanyia upekuzi, uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
Ayo TV & Millardayo.com imempata Baba mzazi wa Marehemu wa Askari aliyejinyonga Mahabusu kafunguka mwanzo mwisho.