Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ni kweli kwamba sasa hivi usalama umeimarika nchini Tanzania kwa ajili ya Mabasi kufanya safari zake usiku na mchana lakini atawasiliana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuona wamejiridhisha kiasi gani ili mabasi yaanze kuruhusiwa kusafirisha abiria wakati wote ili kuboresha uchumi.