Jaji atupilia mbali mapingamizi kwenye kesi ya mgogoro wa ardhi,utapeli kughushi vyatajwa
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetupilia mbali mapingamizi mbalimbali yaliyowekwa na wadaiwa likiwemo la ukomo wa muda wakufungua mashauri ya ardhi.
Wakili anayewakilisha wadaiwa alidai kwamba shauri hilo limefunguliwa nje ya muda wa miaka 12 kwa mashauri ya ardhi.
Mapingamizi hayo yaliyowekwa na Wadhamin wa Jamuiya ya Kiislamu ya Ahlul Bait Centre na Ansaarul Imamiyah pamoja na sheikh Abdlulrazak Amir Msuya.
Akitoa uamuzi huo, Muheshimiwa Jani B.K Phillip baada ya kuwasikiliza mawakili wa pande zote mbili juu ya mapingamizi hayo alitoa maamuzi madogo akiyatupilia mbali mapingamizi hayo akieleza kuwa, panapokuwa na madai ya ghushi, utapeli na udanganyifu mahakama Ina jukumu pekee la kusikiliza shauri hilo na kubaini utapeli, ghushi na udanganyifu unaolalamikiwa na kutoa hukumu yake.
Mahakama iliridhika na hoja za mdai kuwa alichotakiwa kuonyesha kwenye hati ni madai tuu na siyo kuthibitisha.
Katika shauri hilo, Wadaiwa walipinga madai hayo na kuleta mapingamizi ya awali ya kisheria ambapo Mapingamizi yaliyotolewa yalikuwa ni juu ya ukomo wa muda wa kisheria wa kufungua mashauri ya ardhi ambayo huwa yanahitajika kufunguliwa ndani ya miaka 12 tangu kuibuka kwa mgogoro huo ambapo Wadaiwa hao walidai kuwa shauri lililofunguliwa na mdaiwa limefunguliwa nje ya muda hivyo mahakama ifute au kulitupilia mbali shauri hilo
Mdai ambaye ni Zainab Husein Larusai na wenzake walifungua shauri hilo wakilalamika kuwa kiwanja ambamo ulijengwa msikiti wa Answaarul Immamiya hakuwahi kutoa wakfu wa kiwanja Naomba 39 kilichopo mkoani Arusha Mjini Kati ulipo msikiti
Na kwamba uhamisho wa kiwanja hicho kwenda kwa Ahlul Bait Centre umezungukwa na utapeli, udanganyifu na ghushi.
Shauri hilo limeahirishwa hadi February 23 2022 kwa ajili ya maelekezo mengine ya kimahakama