Nchi za Ushirikiano wa Mpito wa Bonde la Mto Nile zimeshauriwa kutochukua maamuzi na hatua za pekee yake badala yake zitumie njia ya mazungumzo ya pamoja katika kutafuta suluhu ya changamoto mbalimbali zinazokabili mataifa hayo.
Dk Philip Mpango ametoa ushauri huo leo wakati wa Maadhimisho ya 16 ya Siku ya Bonde la Mto Nile yaliyofanyika mkoani Dar es Salaam ikiwa ni mara ya pili kufanyika nchini baada yam waka 2017 kufanyika maadhimisho ya 11.