Ni Feb 26, 2022 ambapo Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ametembelea ofisi ya Magilatech yenye tawi lake Dubai.
Magilatech Ni kampuni ya utengezaji na ulinzi wa mifumo ya kidigital ,imejikita zaidi kwenye utengezaji wa Mifumo au Technologia za Malipo, Mawasiliano na Elimu na kwenye Ulinzi wa Mifumo imekuwa ikitoa huduma ya kulinda mifumo kwa kuidukua kabla ya wadukuzi nakuziba njia.
Akizungumza Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw.Godfrey Magila mwenye umri wa miaka 30 anasema kampuni hiyo Yenye Makao Makuu yake alianzisha mnamo mwaka 2012 katika Atamizi ya Tume ya Science na Technologia (Costech) ambapo mpaka sasa wameshatoa ajira kwa vijana 125 ndani na nje ya Nchi wakihudumia nchi mbalimbali ikiwemo Congo, Dubai, Zambia na Eswatini.
Ayo TV & Millardayo.com imekusogezea ushuhudia Msemaji wa Serikali alipotembelea ofisi zake zilizopo Dubai.