Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pa ni Kamanda wa Majeshi ya Nchi kavu ya Uganda ametoa kauli ya kuunga mkono uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika “Watu wengi (ambao sio Wazungu) wanaunga mkono msimamo wa Urusi nchini Ukraine, Putin yuko sahihi kabisa”
“Wakati USSR ilipoweka makombora yenye silaha za nyuklia nchini Cuba mwaka 1962, Nchi za Magharibi zilikuwa tayari kulipua ulimwengu juu yake, sasa NATO ikifanya hivyo wanatarajia Urusi kufanya tofauti!?”
Jenerali Kainerugaba ndiye Afisa Mkuu wa Kwanza wa Kijeshi Afrika kuunga mkono hadharani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Jenerali huyo anatajwa kuwa anaweza kuwa Rais wa Uganda katika siku za usoni na kumrithi Baba yake mwenye umri wa miaka 77 ambaye amekuwa madarakani tangu 1986.