Wamiliki wa meli ya mizigo za Estonia wanasema kuwa imezama katika pwani ya Ukraine baada ya mlipuko.
Wanasema wafanyakazi wawili wamepatikana kwenye viokozi baharini na wengine wanne hawakupatikana wote sita baadaye walichukuliwa na huduma ya uokoaji ya Ukraine.
Meli hiyo yenye bendera ya Panama inamilikiwa na kampuni ya Vista Shipping Agency yenye makao yake huko Estonia. Jimbo la Baltic Estonia ni mwanachama wa Nato na ina mpaka na Urusi.
Meli hiyo ilikuwa imetia nanga katika pwani ya Ukraine baada ya kuondoka katika bandari ya kusini ya Chornomorsk karibu na Odesa siku kadhaa zilizopita.
Haijabainika ni nini kilisababisha mlipuko huo.
Jeshi la Ukraine linasema kuwa Urusi inatuma meli za kutua ili kukamata Odesa, jiji la watu milioni moja na bandari kuu, wakati inaendelea kusonga mbele kusini mwa Ukraine.