Urusi limekuwa taifa linaloongoza kwa kuwekewa vikwazo vingi zaidi ulimwenguni ikiipiku Iran wakati mataifa ya magharibi yaliliwekea maelfu ya vikwazo vinavyolenga makampuni ya Urusi na watu binafsi kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine.
Taarifa hii ni kulingana na taasisi ya kimataifa inayofuatilia vikwazo ya Castellum.Al ya nchini Marekani.
Urusi imewekewa karibu vikwazo 4,000 tangu Februari 22 siku moja baada ya rais Vladimir Putin kutambua maeneo ya waasi wanaotaka kujitenga mashariki mwa Ukraine kuwa ni mataifa huru na kuagiza wanajeshi kupelekwa kwenye eneo hilo.
Kabla ya Februari 22 Urusi ilikuwa na vikwazo chini ya 3,000 na vingi miongoni mwa hivyo vilifuatia hatua yake ya kuinyakua Rasi ya Crimea mwaka 2014. Iran ina vikwazo 3,600 ilivyowekewa kutokana na mipango yake ya nyuklia na kuunga mkono makundi ya kigaidi.