Kutoka Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu Mbunge Fatma Hassan Toufiq ametaka kujua idadi ya wahanga wa vitendo vya ukatili nchini kuanzia mwaka 2019 hadi 2022.
Akijibu swali hilo Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema Takwimu za matukio ya vitendo vya ukatili nchini vilivyoripotiwa kwenye vituo vya Polisi kuanzia mwaka 2019 hadi machi, 2022 ni 27,838 kwa mchanganuo ufuatao: matukio ya kubaka ni 19,726, kulawiti ni 3,260 kati yao wanaume 3,077 na wanawake 183, kuunguzwa kwa moto ni 198 kati yao wanaume 73 na wanawake 125, kutupa watoto wachanga ni 443 kati yao wanaume 177 na wanawake 266, kipigo ni 4,211 kati yao wanaume 16 na wanawake ni 4195.
Aidha ameongeza kuwa jumla ya kesi zilizofikishwa Mahakamani ni 21,063 na watuhumiwa waliohukumiwa ni 14,278 na mashauri mengine yako kwenye hatua mbalimbali za upelelezi na mahakamani. Aidha, Serikali inaendelea kuiasa jamii kutumia vema taasisi za familia, kaya, jumuiya za kidini na ngazi za vitongoji, vijiji na mitaa kudhibiti vitendo vya ukatili katika jamii.
MBUNGE MUSUKUMA AIBUKA NA BUNGE LIVE ‘KUNA WABUNGE VILAZA, SIO KUONGEA KINGEREZA BILA SABABU