Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Deus Seif amesema Walimu walionufaika kwa kupandishwa madaraja (vyeo) katika Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu katika kipindi cha mwaka 2021/2022 pekee ni 92.9% ya Walimu wote ambao ni takribani 260,000.
Deus ametoa kauli hiyo akiwa Mwanza leo ambapo amesema “Ajira imetolewa kwa awamu nne, ya kwanza Walimu 13,000, ya pili 7000, ya tatu 6000 na ya nne ni hii ya juzi 12,000 kwa harakaharaka ni sawa na 15% ya Walimu waliopo”
“Kwa upande wa madaraja (vyeo) mwaka jana Walimu 127,000 wamepanishwa vyeo, mwaka huu zajdi ya 60,000, watakaonufaika na daraja la mserereko ni Walimu 52,0000 ambapo kwa haraka jumla ya walionufaika ma madaraja ni sawa na 92.9%”
“Ukiacha miundombinu ya madarasa/samani na vitabu tayari TAMISEMI imeanza zoezi la ujenzi wa nyumba za Walimu, unaachaje kusema asante kwa Mh. Rais kwa hatua hii kubwa kwa Walimu, Asante Mama”
RAIS SAMIA KAMA OBAMA KWENYE ROYAL TOUR, “AMEJIACHIA SANA, WOOH”