Halmashauri 144 kati ya 184 zilizoko Tanzania bara zimenufaika na mafunzo endelevu ha Walimu Kazini (MEWAKA) ili kuwajenge uwezo Walimu katika utoaji wa elimu bora na kuendana na uboreshaji wa Elimu unaoendelea nchi nzima.
Mratibu wa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini(MEWAKA) Cosmas Mahenge amesema, mpaka sasa Walimu kutoka Halmashauri takribani 122 zimeshapatiwa mafunzo hayo na sasa wanamaliza katika Kanda ya Ziwa na Magharibi.
Mahenge ameleeleza hayo Mkoani Kagera wakati akiongea na walimu wakati wa kufungua mafunzo hayo Ana kueleza kuwa mafunzo hayo yamelenga walimu wa shule ya awali na msingi lengo ni kuwaendeleza kitaalam na kitaaluma kuwapa mbinu za ujifunzaji na ufundishaji na jinsi ya kuweza kutatua changamoto wanapokuwa katika vituo vya kazi.
Amesema mafunzo ya MEWAKA mbali ya kujifunza mbinu za ujifunzaji na ufundishaji yatamsaidia mwalimu kuendana na mbabiliko yanayotokea katika elimu na jamii tunayoishi na walimu ni lazima wabadilike.
“Niwaombe walimu pamoja na kuendelea kwamafunzo haya yasiathiri ratiba za kufundishia madarasani hivyo kila mmoja asingatie sheria, kanuni na taratibu za mafunzo na tuwe mabolozi wazuri kwa walimu wenzetu na wanafunzi wetu tunaowasimamia” amsesema Cosmas
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Wawezeshaji wa MEWAKA Bw. Ferdinand Mlandali amesema, maufunzo yatamsaidia mwalimu kujifunza na kuendana na mabadiliko ya sekta ya elimu.
Walimu watawezeshwa kujua njia za kufunza ikiwemo mitaala na kumsaidia kuendana na karne ya 21 ikiwa ni pamoja na mawasiliano, ubunifu, namna ya kujifunza kwa pamoja ili kuwasaidia wanafunzi hata wanapo rudi nyumbani waweza kufanya vizuri.
Aidha, amesema mafunzo haya pia yatamuwezesha mwalimu kujua njia ya “learning management system” na kuweza kujifunza kutumia maktaba mtandao kwa kuweza kupakua/kupata na materials mbalimbali.
Naye Sista Felista Pamerace(Mwl.Shule ya Msingi Mwemage) amesema, wapo tayari kujifunza na kuelekezwa na kuwa mabalozi wazuri wa walimu wenzao kwa kuwaelekeza na kwa wanafunzi kuweza kuwafundisha.