Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA) imeeleza kuwa imejipanga kikamilifukusimamia mradi wa kubadili gesi asilia kuwakimiminika (LNG) ili kuhakikisha mradi huo unaletatija na kuchangia maendeleo ya uchumi nchini.
Hayo yamesemwa na Mjiolojia Fortunatus Kidayialipokuwa akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa waLindi, Mhe. Zainab R. Telack aliyetembelea banda la PURA katika Maonesho ya Tano ya Mifuko naProgramu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumiyanayoendelea mkoani Morogoro.
Alifananua kuwa miongoni mwa majukumu ya PURA kwa mujibu wa Sheria ya Petroli ya mwaka 2015 nikusimamia mradi wa LNG. Mradi huu unalengakuvuna gesi asilia iliyogunduliwa kina kirefu cha bahari nchini kwa ajili ya matumizi ya ndani na kiasikingine kuuzwa nje ya nchi.
“Mradi huu ni wa thamani ya Dola za Marekani bilioni30 na unatarajiwa kutekelezwa eneo la Likong’omkoani Lindi na PURA imeendelea kujiimarishakiutendaji ikiwemo kuendelea kuwajengea watumishiwake uwezo katika eneo la LNG” alieleza Bw. Kidayi.
Aliongeza kuwa PURA imejipanga kuhakikishaWatanzania wanapata fursa ya kushiriki katika mradiwa LNG kupitia ajira na utoaji wa huduma na bidhaakatika kipindi chote cha utekelezaji wake.
“Katika kufanikisha hilo, PURA kwa kushirikiana naEWURA imeandaa kanzi data ya kuwasajili watoahuduma wa Kitanzania na wazawa wenye taalumambali mbali ikiwemo masuala ya mafuta na gesi. Kanzidata hiyo inajulikana kwa jina la Common Qualification System (CQS) na iko tayari kutumika,” alibainisha.
Aliongeza kuwa “mradi wa LNG unatarajiwa kuletafursa nyingi nchini ikiwa ni pamoja na ajira zaidi 6,000 na ikiwa ni pamoja na fursa za kuuza bidhaa nahuduma wakati wa utekelezaji wa mradi huo. Serikaliilishatoa Shilingi bilioni 5.7 kulipa fidia kwa wananchizaidi ya 640 waliopisha utekelezaji wa mradi. Aidha, majadiliano baina ya Serikali na kampunizitakazotekeleza mradi wa LNG yanaendelea nayanatarajiwa kukamilika hivi karibuni“.
Kwa upande wake, Mhe. Telack ameipongeza PURA kwa kusimamia suala ushiriki wa Watanzania kwenyeshughuli za mkondo wa juu wa petroli, na kusemakuwa wananchi wa mkoani humo wanasubiri kwahamu kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo nakwamba ana imani watapewa kipaumbele wakati wautekelezaji wake.